08 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Jitihada zinaendelea kuwafutia kesi wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 
2008-05-08 14:29:13
Na EAR Habari

Wakati uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania, ukiwa katika jitihada za kufuta kesi inayowakabili wanafunzi wake waliosimamishwa masomo kwa kutuhumiwa kufanya vurugu mwezi uliopita, imeelezwa kuwa sheria hairuhusu kufanya hivyo.

Vyombo mbalimbali vya habari vimemkariri Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Yunus Mgaya, akiwataka wanafunzi hao kurejea chuoni kwa maandalizi ya kufanya mitihani inayotarajiwa kuanza Mei 19 mwaka huu.

Lakini mwanasheria katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu amesema kwamba, mamlaka yenye uwezo wa kufuta kesi ya jinai ni Jamhuri ya Muungano.

  • SOURCE: EAR
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.