|
Shule za sekondari nchini Uganda kupandisha ada kuanzia muhula ujao
2008-05-08 14:29:56
Na EAR Habari
Shule za sekondari nchini Uganda inasemekana zimepandisha ada kuanzia muhula ujao, kutokana na ongezeko la bei ya chakula hivi karibuni.
Wengi wa waalimu wakuu kutoka shule mbali mbali wamesema kuwa, kamati za utawala ziliidhinisha mfumo mpya wa ada ,muhula uliopita wa shule.
Shule ambazo hazijaongeza ada inasemekea zimeiandikia wizara ya elimu nchini humo, zikiomba kibali cha kuongeza ada, huku nyingine zikitaarifu kwamba zitapunguza baadhi ya shughuli ili kutoa huduma kwa wanafunzi.
|