|
Watimishi wa serikali nchini Kenya kupewa nyongeza ya mishahara
2008-05-08 14:30:54
Na EAR Habari
Waziri wa utumishi nchini Kenya Mh. Dalmas Otieno, amesema kwamba serikali itatoa shillingi billioni 3.5 ikiwa ni nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa serikali, kuanzia mwezi julai ili kuwa na uwiano.
Fedha hizo zitatumika kwa kuandaa utaratibu mpya uliobuniwa na bodi ya utumishi wa umma ya mishahara, ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano sawa wa mishahara kwa watumishi wa serikali.
Habari zinasema ingawa waziri hakutangaza asilimia atakayopata mfanyakazi wa kima cha chini, lakini kutolewa kwa fedha hizo kunamaanisha kuongezeka kwa mishahara kwa watunmishi wa kiwango cha A mpaka M.
|