|
Wanaume wengi hupendelea kuoa wanawake wenye fedha Uingereza
2008-05-09 16:32:41
Na EAR Habari
Utafiti uliofanyika nchini Uingereza umebainisha kwamba wanaume wengi hupendelea kuoa kwa ajili ya kunufaika kifedha ingawa imekuwa ikionekana kuwa wanawake huolewa kwa kufuata fedha.
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 19 ya wanaume wamekubali kuwa watafutaji wa mali na wangekuwa tayari kumuoa mwanamke mwenye uwezo waweze kunufaika kutoka na mali zake dhidi ya asilimia 11 ya wanawake.
Wakati asilimia 67 ya wanawake wanasema kwamba ni muhimi kujipatia fedha zao wenyewe,wakati asilimia 76 hawategemei wenza wao kuchukua nafasi ya maamuzi katika masuala ya fedha.
|