|
Chama cha MDC hakimtaki Mugabe kuwa sehemu ya makubaliano
2008-05-09 16:36:27
Na EAR Habari
Katibu mkuu wa chama cha MDC nchini Zimbabwe Tendai Biti amesema kwamba rais Robert Mugabe hatakiwi kuwa sehemu ya makubaliano yatakayo fikiwa kufuatia uchaguzi nchini humo na lazima aondoke.
Akiongea katika ukumbi uliokuwa umefurika wasikiliozaji kastika semina iliyokuwa imeandaliwa na taasisi ya kituo cha haki na usuluhishi amesema huu ni wakati wa kiongozi huyo kuondoka.
Chama cha MDC kimezishutumu nchi za jumuia ya maendeleo ya nchi zilizoko kusini mwa Africa SADC na jumuia ya kimataifa kwa kushindwa kusaidia mabadiliko nchini Zimbabwe.
|