|
Ashikiliwa na polisi Tanzania kwa kusafirisha Wasomali wasio na vibali
2008-05-09 16:37:04
Na EAR Habari
Jeshi la Polisi nchini Tanzania linamshikilia mkazi wa Himo Moshi, Mkoani Kilimanjaro, William Makina baada ya kukutwa akisafirisha raia 34 wa Somalia ambao hawakuwa na vibali vya kuingia wala kuishi nchini.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania Thobias Andengenye, zilisema Makina, alikamatwa jana, majira ya jioni na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika eneo la Dumila wilayani Kilosa, katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma.
Alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akiendesha lori aina ya Fuso namba T 315 ADM lililokuwa likitokea Kiteto mkoani Manyara kuelekea jijini Dar es Salaam na kwamba dereva huyo na raia hao wa Kisomali watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za upelelezi kukamilika.
|