|
Uganda kumtangaza mwanafunzi Yvonne Namaganda kama shujaa wa taifa
2008-05-09 16:39:52
Na EAR Habari
Bunge nchini Uganda limepitisha hoja iliyowasilishwa bungeni ya kumtangaza mwanafunzi Yvonne Namaganda kuwa shujaa wa taifa, Yvonne alikufa wakati akiwaokoa wanafunzi wenzake katika janga la moto lililotokea katika shule ya Budo.
Hoja hiyo ambayo iliwasilishwa na mbunge mwakilishi wa wanawake jimbo la Wakiso Rosemary Seninde wa chama cha NRM ambaye shule ya Budo iko katika jimbo lake,ulipokelewa kwa pamoja na wabunge kutoka vyama mbali mbali.
Wanafunzi 20 wenye umri kati ya miaka minne mpaka kumi walikufa baada ya shule hiyo kuungua moto tarehe 14 mwezi April na mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijulikani.
|