15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Shea ya chakula kwa wanafunzi wa chuo cha Makerere yapunguzwa
 
2008-05-15 17:19:13
Na EAR Habari

Ongezeko la bei ya chakula limevuruga bajeti ya Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, na kusababisha utawala wa chuo hicho kupunguza shea ya chakula kwa wanafunzi.

Pamoja na kupunguza kiwango cha mlo unaotolewa, chuo hicho pia kimebadili aina ya chakula kinachotolewa.

Mkuu wa Wanafunzi John Ekudu, amefafanua kuwa chuo hicho kinafanya kila jitihada kumaliza tatizo hilo, na kuhakikisha wanafunzi hawali chakula cha aina moja kwa muda mrefu.

Hivi sasa wanafunzi hao wanapatiwa ugali na maharagwe tu badala ya vyakula mchanganyiko.

  • SOURCE: EAR
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.