|
Watu zaidi ya 50,000 wahofiwa kufa katika tetemeko nchini China
2008-05-16 15:23:27
Na EAR Habari
Rais wa China Hu Jintao yuko kusini magharibi mwa jimbo la Sichuan lililokumbwa na tetemeko na kusababisha maafa makubwa na ikihofiwa kuwa zaidi ya watu 50,000 wamekufa.
Shirika la uitangazaji la nchi hiyo Xinhua limesema kuwa watu 20,000 wamedhibitika kupoteza maisha katika jimbo hilo wakati maelfu ya watu hawajulikani walipo.
Rais Hu amesema kazi ya uokoaji imeingia katika hatua muhimu huku wakiendelea kuondoa mabaki ya nyumba zilizoanguka wakiwa na matumaini ya kuwapata watu wakiwa hai.
|