|
Waasi wa RUF walikuwa wakatili kwa kuwakata viungo raia
2008-05-16 15:28:14
Na EAR Habari
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor ambaye anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu wa kivita inasemekana alikataa malalamiko kutoka kwa waasi wa Sierra Leone juu ya uhalifu uliokuwa ukifanywa na askatri wake.
Akitoa ushahidi katika mahakama ya uhalifu ya kimataifa huko the Hague, makamu wake wa zamani Moses Blah amesemakuwa waasi wa RUF walikuwa wakatili kwa kuwakata viungo raia ingawa kiongozi wao Foday Sankoh alimlalamikia Taylor juu ya vitendo hivyo vya askari wa Liberia.
Blah amesema kwamba baada ya Tailor kuambia hivyo alitishia kuyaondoa majeshi yake, Blah ambaye alichukua madaraka kwa muda mfupi anakuwa kiongozi wa kwanza mwandamizi kutoa ushahidi.
|