|
Mashindano ya mpira wa kikapu kwa vijana chini ya umri wa miaka 14 na 18 yamemalizikia
2006-07-10 11:49:53
By ITV Habari
Mashindano ya mpira wa kikapu kwa vijana chini ya umri wa miaka 14 na 18 yamemalizikia jana jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa wasichana chini ya umri wa miaka 14, ubingwa umechukuliwa na timu ya Ali Hassan Mwinyi baada ya kuifunga timu ya Don Bosco vikapu 10-3.
Kwa upande wa wavulana chini ya umri wa miaka 14 ubingwa umechukuliwa na Don Bosco baada ya kuifunga JKT vikapu 24-14 na kwa upande wa wavulana chini ya umri wa miaka 18 ubingwa umechukuliwa na TM Rocekts baada ya kuifunga Don Bosco vikapu 45-26.
Mashindano hayo yameandaliwa na chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na shirika la michezo kwa vijana- Emima yalishirikisha jumla ya timu 18 za shule za msingi pamoja na vilabu.
|