|
Michuano ya ligi daraja la kwanza netiboli imeendelea jana
2006-07-10 11:50:29
By ITV Habari
Michuano ya ligi daraja la kwanza netiboli imeendelea jana kwenye viwanja vya gerezani kwa timu ya JKT Mbweni kuifunga Polisi Mara, magoli 45-33 wakati Polisi Morogoro nayo imeifunga Polisi mara magoli 46-35.
Katika mchezo mwingine manispaa ya ilala imeifunga Magereza Chuo, magoli 65-28 wakati magereza Morogoro iliifunga CMCU magoli 56-34.
Katika mechi zilizochezwa mchana timu ya Mapinduzi Dodoma iliifunga Polisi Arusha magoli 45-27.
|