|
Mdahahalo wa kitaifa kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi wamalizika
2008-05-13 10:57:32
Na ITV Habari
Mdahahalo wa kitaifa kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi umemalizika kote nchini kukiwa na matumaini ya mabadiliko ya kiuchumi kupitia mikakati ya kanda za mikoa mbalimbali waliyojiwekea.
Katika mdhahalo uliofanyika kanda ya kati wakuu wa mikoa hiyo wamesema mbali ya kuwepo bajeti ya uwezeshaji wananchi kila mwaka changamoto kubwa ni kwa watendaji katika asasi za fedha kuwezesha wanachi kufikiwa na huduma hizo kwa wakati bila urasimu mwingi.
Kwa upande wake katibu mtendaji baraza la taifa la biashara TNBC Bw. Dunstan Mrutu amesema kufanikiwa kwa mkakati huo kutategemea zaidi jitihada za watendaji katika maeneo yao.
|