|
Tanzania kupambana na vikwazo vinavyoshusha bei ya kahawa duniani
2008-05-13 10:58:25
Na ITV Habari
Tanzania imetakiwa kuhakikisha inapambana ipasavyo kuondoa vikwazo vya kibiashara vinavyochangia kushuka kwa mauzo ya kahawa katika soko la dunia na kuweka mikakati ya kupambana na tatizo hilo.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na masoko Dr. Stergomena Tax Bamwenda wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya kahawa wanaokutana kujadili mkakati wa kuisaidia tanzania kushiriki katika uboreshaji wa mauzo ya zao la kahawa.
Kwa upande wake dalali wa zao la kahawa kutoka bodi ya kahawa nchini Bw. Elia Mkwawa amesema Tanzania inauza karibu asilimia 90 ya zao la kahawa nje ya nchi na kuwataka wakulima kuweka mbinu mbadala za uzalishaji wa kahawa kwa ubora unaokidhi soko la nje.
|