14 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Tanzania leo imezindua baraza la nafaka
 
2008-05-14 15:03:50
Na ITV Habari

Tanzania leo imezindua rasmi baraza lake la nafaka la afrika mashariki ambalo litakuwa likisaidiana na nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuainisha changamoto zinazowakabili wakulima na namna ya kusaidia kuboresha zao la nafaka kwa nchi wanachama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwenyekiti wa baraza hilo bwana Nick Hutchinson amesema wameamua kuzindua baraza hilo hapa tanzania ili kuboresha hali ya nafaka kwa nchi za jumuiya chini ya mpango wa utekelezaji wa programu hiyo kwa wafadhili na kudhibiti mfumuko wa bei ya nafaka kwa nchi za Afrika Mashariki.

Mapema wadau wa baraza hilo kutoka nchi za Kenya na Tanzania wamesema kuwa kupanda kwa bei ya nafaka katika dunia kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuwepo mahitaji makubwa ya nafaka kuliko uwezo wa kuzalisha, pamoja na kuuza ziada kuliko kuhifadhi nafaka.





  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.