|
Membe aelezea umuhimu wa mkutano wa Sullivan
2008-05-14 15:04:30
Na ITV Habari
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimatiafa Mhe. Bernard Membe amesema mkutano wa nane wa Sullivan utatoa fursa za uwekezaji, biashara utalii na utajenga msingi wa ushirikiano wa utalaamu.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya udhamini wa mkutano wa sullivan yenye thamani ya dola laki moja kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo kutoka benki ya CRDB waziri Membe amesema benki ya CRDB ndio itakayotoa huduma za kibenki katika mkutano huo.
Naye mkurugeni wa CRDB Dk. Charles Kimei amesema wanathamini mkutano huo kwa sababu utaleta faida kubwa kwa wafanyabiashara wa hapa nchini na maendeleo ya watanzania.
|