|
Wachimbaji wadogo wa dhahabu kuwekewa kiwango cha matumizi ya zebaki
2008-05-14 15:07:10
Na ITV Habari
Shirika la viwango Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka wizara ya nishati na madini wamekubaliana kuweka kiwango kitakachokuwa kikitumika kudhibiti matumizi ya madini ya zebaki yanayotumiwa na wachimbaji wadogo kusafishia dhahabu.
Wakizungumza wakati wa mjadala wa kukamilisha kiwango hicho ambacho kitaanza kutumika hivi karibuni, mwenyekiti wa kamati ya viwango Bi Angelina Madete amesema kwa sasa wameaanza kuanishisha mwongozo utakaotumiwa ili kupunguza athari za madini ya zebaki yanayotumiwa kusafisha madini na kuharibu vyanzo vya mito na maji.
|