|
Wavu Afrika Mashariki na Kati kuanza Mei 28
2008-05-15 10:57:53
By ITV Habari
Timu za mpira wa wavu za Jeshi Stars na Magereza ambazo zitashiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati kuanza Mei 28 - June 1 zimeendelea na mazoezi mepesi kabla ya kuondoa kulekea nairobi nchini Kenya ambapo zitapambana na timu kutoka Uganda, Rwanda, Burundi, Kongo na wenyeji Kenya.
Akizungumza katika uwanja wa ndani wa taifa kocha wa timu ya Jeshi Stars Lameck Mashindano amesema pamoja na mazoezi waliyofanya timu yake haikufanikiwa kupata mechi ya majaribio ili kujipima nguvu kabla ya mashindano hayo.
|