15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kampuni ya ndege ya Precision Air kuongeza safari za ndege zake
 
2008-05-15 11:00:53
Na ITV Habari

Kampuni ya ndege ya Precision Air imesema itaongeza safari za ndege zake kutokana kuwepo kwa ndege mpya aina ya Boing 737 Dashj 300 iliyokodishwa kutoka nchini Ireland na kuanza kutoa huduma zake hapa nchini.

Meneja ubora na usafiri kutoka shirika hilo Bw. Allen Sharra amesema kwa sasa ushindani katika sekta ya usafiri wa anga umekuwa mkubwa, na kinachotakiwa ni kutoa huduma bora kwa wateja na kuhakikisha wanajipanga vema kukabiliana na ushindani.

Kwa sasa shirika hilo lina jumla ya ndege 9 zinazotoa huduma katika mikoa mbalimbali hapa nchini, na kuongeza kuwa ujio wa ndege hiyo utaongeza safari za shirika hilo katika nchi za Rwanda, Angola, Lubumbash, na Johannesburg.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.