15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Tanzania huenda ikanufaika na mkutano wa 8 wa Leon Sullivan
 
2008-05-15 11:02:59
Na ITV Habari

Tanzania iwapo itatumia vema nafasi ya uenyeji wa mkutano wa nane wa Leon Sullivan huenda ikanufaika na miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo ile ya uzalishaji umeme, utalii na usindikaji kutoka kwa wafanyabiashara wawekezaji wa Marekani weusi.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti mwenza wa kamati ya maandalizi ya sullivan kutoka taasisi ya Sullivan ya Marekani Bw. Carlton Masters wakati akizunguzma na waandishi wa habari juu ya mkutano wa nane wa mwaka huu wa Sullivan ambao kwa sasa Tanzania inajiandaa na ugeni huo wa wafanyabiashara wapatao 500 kutoka Marekani.

Akizungumzia umuhimu wa Tanzania kama mwenyeji wa mkutano huo Bwana Masters amesema wafanyabiashara wa marekani wako tayari kufanya biashara na wenzao wa tanzania katika sekta mbalimbali na kuipongeza Tanzania kwa jitihada zake za kukuza uchumi na kupunguza umaskini .

Bwana Masters ambae alikuwa ameongozana na wanakamati kadhaa wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa nane wa Sullivan unaotarajia kuanza tarehe 2 hadi tarehe 6 mwezi ujao amesema ameridhishwa na maandalizi ya Tanzania katika kufanikisha mkutano huo wa kihistoria.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.