15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Reppsi wamezindua kitabu cha kufahamu mwenendo wa mwili kwa wanaoishi na virusi vya ukimwi
 
2008-05-15 11:06:41
Na ITV Habari

Wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali Reppsi wamezindua kitabu kitakachowawezesha wanaoishi na virusi vya ukimwi kufahamu mwenendo wa mwili pamoja na upangaji wa malengo ya maisha.

Meneja wa kanda shirika la Reppsi Bw. Peter Masesa amesema lengo kuu la uzinduzi wa kitabu hicho ni kuhakikisha watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wanapata fursa ya kuelewa na kuweka kumbukumbu za miili wakati mabadiliko yatakapojitokeza na kuyatafutia ufumbuzi kwa madaktari.

Nae mwakilishi wa tume ya kudhibiti ukimwi- Tacaids Bw. Jumanne Sangu na wadau wengine wamezitaka tasisi zinazojishughulisha na masuala ya ukimwi kushirikiana katika kuendeleza vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ili kuokoa nguvu kazi iliyohatarini kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.