|
TCRA imetoa leseni kwa makampuni matano kwa ajili ya utoaji huduma za mawasiliano
2008-05-15 11:07:44
Na ITV Habari
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania-TCRA imetoa leseni kwa makampuni matano kwaajili ya utoaji huduma mbalimbali za mawasiliano.
Akitoa leseni hizo jijini Dar es Salaam jana, mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Prof. John Nkoma amewataka wenye makampuni wazingatie kutoa huduma yenye kiwango bora.
Kwa upande mwingine baadhi ya washiriki wa maonyesho ya teknolojia ya mawasiliano yanayoendelea jijini , wamesema watanzania wanaonekana kuwa na ari ya kwenda sambamba na teknolojia mpya za mawasiliano kutokana na kujitokeza kwa wingi kutaka kujua teknolojia mbalimbali.
|