15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Nchi za Afrika zitaathirika zaidi kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
 
2008-05-15 11:09:01
Na ITV Habari

Nchi za Afrika zitaathirika zaidi kutokana na mabadiliko ya tabia nchi licha ya kuchangia kidogo sana katika tatizo hilo ambalo athari zake ni pamoja na ukame, mafuriko na vimbunga.

Mkurugenzi wa mazingira katika ofisi ya makamu wa rais Bw. Erick Mugurusi amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya siku ya mazingira yanayofanyika Juni 5 kila mwaka ambapo amesema kazi iliyopo ni kwa nchi za afrika kushiriki katika kuzishinikiza nchi zilizoendelea kupunguza uzalishaji wa gesi ili kuepusha athari zake.

Kauli mbiu ya mwaka huu kidunia ni badili mazoea , jenga uchumi endelevu kwa kudhibiti uzalishaji gesi joto- huku kauli mbiu ya kitaifa ni hifadhi mazingira , dhibiti uchomaji moto, panda miti.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.