|
Leo ni siku ya wanafamilia
2008-05-15 11:10:14
Na ITV Habari
Leo ni siku ya wanafamilia ambapo watanzania wameshauriwa kuwa na mshikamano miongoni mwa familia zao ili waweze kukabiliana na hali ngumu zinazozikabili familia katika jamii.
Ushauri huo umetolewa na waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Mh. Magreth Sitta ambaye amesema serikali katika kujali suala la wanafamilia imechukua hatua za kuzisaidia familia nchini kwa kutunga sera ya kukabiliana na matatizo ya kijamii hasa la kupiga vita mila desturi na tamaduni zilizopitwa na wakati.
Sherehe ya wanafamilia inaadhimishwa katika ngazi ya mkoa ikiwa na kauli mbiu inayosema kina baba na familia majukumu na changamoto.
|