|
Mashabiki wa soka zaidi ya 400 waenda Kampala
2008-05-16 14:19:55
By ITV Habari
Mashabiki wa soka zaidi ya 400 kutoka mkoa wa Kagera wataondoka leo kwenda Kampala nchini Uganda kuishangilia timu ya soka ya Tanzania- Taifa Stars ambayo imeondoka jana kwenda huko kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano na timu ya taifa ya Uganda The Cranes.
Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Enos Mfuru ameeleza hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wachezaji wa timu ya mkoa wa Kagera- Rwelu Eagles inayoshiriki mashindano ya Sarafi Lager taifa Cup na kutoa wito kwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa michuano hiyo inayooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV kwa kuwa wanafuatiliwa vizuri na wenzao nyumbani.
Mapema mkuu wa msafara wa timu hiyo inayoendelea katika michuano hiyo baada ya kuitoa timu ya mkoa wa Tanga na Ruvuma na viongozi wengine wameahidi zawadi nono kwa timu hiyo.
|