|
Asilimia 10 ya wananchi wanatumia huduma za benki
2008-05-16 14:24:21
Na ITV Habari
Waziri wa nchi anayeshughulikia fedha na uchumi katika ofisi ya rais ya serikali ya mapinduzi Zanzibar Dr. Mwinyi Makame amesema hadi sasa ni asilimai 10 ya wanachi ndio wanaotumia huduma za taasisi za fedha nchini hali ambayo inaashiria kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya matumizi ya huduma hizo kwa jamii.
Ametoa kauli hiyo katika mkutano wa kimataifa wa nchi za Afrika kuhusu matumizi ya huduma za benki kisiwani Zanzbar ambapo amesema shughuli za huduma za kifedha zinahitaji mabadiliko makubwa kwa kutumia vifaa vya kisasa vitakavyotosheleza mahitaji ya kijamii badala ya utaratibu wa sasa kuwa katika maeneo machache.
Naye mtendaji mkuu wa benki ya posta nchini Bw. Alfonce Kihwele amesema mkutano huo unatarajia kuleta mabadiliko makubwa katika huduma za kibenki ikiwemo utoaji mikopo bila riba kwa wananchi wa pato la chini na wa vijijini.
|