|
Waandishi wa habari wawili waibuka washindi wa CNN Afrika
2008-05-16 14:27:25
Na ITV Habari
Waandishi wa habari wawili wa Tanzania wameibuka washindi mingoni mwa washindi 23 kutoka nchi 14 walioshiriki shindano la mwandishi bora wa mwaka wa tuzo ya CNN, 2008.
Walioshinda tuzo hiyo kutoka Tanzania ni Mwandoshah Mfanga wa gazeti la The Guardian na Richard Mgamba wa Sunday Citizen.
Matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa majaji wa shindano la tuzo hizo Bw. Azubuike Ishiekwene yanaonesha shindano hilo mwaka huu limevunja rekodi ya kuwa na washiriki wengi ambapo jumla ya washiriki 1912 kutoka nchi 44 barani Afrika walishindania tuzo hizo.
Washindi hao watazawadiwa tuzo zao huko Accra Ghana Jumamosi ya tarehe 19 July.
|