16 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Hospitali ya misheni Iambi inakabiliwa na upungufu wa watumishi
 
2008-05-16 14:28:49
Na ITV Habari

Hopitali ya misheni Iambi iliyopo kata ya Nkungi wilayani Iramba inakabiliwa na upungufu wa watumishi arobaini wa kada ya uuguzi hali inayochangia baadhi ya huduma katika hospitali hiyo kutotekelezwa kwa ukamilifu.

Wauguzi wa hospitali hiyo inayomilikiwa na kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania -KKKT Dayosisi ya kati wamemwambia askofu wa dayosisi hiyo kuwa kwa sasa ina idadi ndogo ya watumishi ikilinganishwa na mahitaji ya huduma ambayo ni mara mbili ya wauguzi arobaini waliopo hivi sasa.

Kwa upande wake askofu wa dayosisi hiyo askofu Eliuphoo Sima amewataka watumishi kutoa huduma kwa kuzingatia upendo, huruma na kuacha tabia ya kubagua watumishi kwa makabila huku akitaka wenye viwango vya chini vya elimu wajiendeleze wakiwa kazini kuboresha taaluma zao.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.