|
Haki za binadamu zilizopo kwenye mikataba ya kimataifa zinaleta ugumu mahakama za Tanzania
2008-05-16 14:33:11
Na ITV Habari
Haki za binadamu zilizopo kwenye mikataba ya kimataifa, hazijafanywa kuwa ni sehemu ya sheria rasmi za kitanzania hali inayoleta ugumu katika utekelezaji wa baadhi ya haki hizo kisheria katika mahakama za Tanzania.
Jaji mkuu wa Tanzania Mhe. Agustino Ramadhani amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha maalum kwa majaji toka nchi nane za Afrika ikiwemo Tanzania kuhusiana na haki za watu wenye ukimwi na wale wenye ulemavu wanavyobaguliwa kutokana na hali zao.
Mapema wawakilishi wa shirika la kazi duniani lililoandaa warsha hiyo wamesema kumekuwepo vitendo mbalimbali vya ubaguzi na unyanyasaji makazini dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na wale wenye ulemavu suala ambalo ni kukiukwa kwa haki za binadamu.
|