16 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

SUMATRA wapiga marufuku daladala kupandisha nauli Dar
 
2008-05-16 14:34:50
Na ITV Habari

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu - SUMATRA imepiga marufuku upandaji holela wa nauli za mabasi ya abiria jijini maarufu kama daladala zinazofanya safari zake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Marufuku hiyo imetolewa na afisa mfawidhi wa SUMATRA kanda ya mashariki Bw. Walakani Luhamba kufatia msako wa kushtukiza uliofanywa na mamlaka hiyo na kukamata daladala korofi zinazotoza nauli kinyume na utaratibu.

Baadhi ya wakazi wa jiji wamekiri kuwepo kwa ongezeko holela la nauli huku baadhi ya makondakta wakidai tatizo hilo linachangiwa kwa kiasi kikubwa na msongamano barabarani.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.