|
Wilbrod Slaa ashinda kesi ya uchaguzi
2008-05-16 14:37:09
Na ITV Habari
Mbunge wa karatu kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Wilbrod Slaa ameshinda kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo baada ya mahakama kuu kanda ya Arusha kutupilia mbali kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa chama cha mapinduzi,CCM ya kuitaka mahakama hiyo itengue matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mbunge huyo.
Jaji Robert Makaramba katika hukumu yake iliyochukuwa saa mbili na nusu alitupilia mbali madai yote ya upande wa walalamikaji ingawa alikubaliana na kuwepo tatizo la kuhesabu kura lililoathri pande zote ambapo hata hivyo Dr. Slaa anabaki na kura nyingi zaidi ya mgombea wa CCM Patrick Tsere.
|