11 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Baraza la Michezo Zanzibar lavunjwa
 
2006-07-11 09:47:03
By Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar Ali Juma Shamuhuna ameujvunja uongozi wa Baraza la Michezo kabla ya kumaliza muda wake kwa maslahi ya kuendeleza michezo visiwani hapa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, Shamuhuna ambaye pia ni Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema ametumia sheria namba 8 ya kuanzishwa kwa Baraza la Michezo ambayo inampa uwezo huo.

Waziri Shamuhuna amewaondoa viongozi wote wa juu waliokuwa wakiongoza baraza hilo pamoja na wajumbe wake wote na kuteua wajumbe wapya wengine.

Viongozi wapya waliochaguliwa ni Mwenyekiti Sherry Khamis ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Zanzibar, CHANEZA, ambaye anachukua nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti ,Abdulghan Msoma.

Aidha, waziri amemteua Khamis Ali Mzee Kichole kuwa katibu wa baraza hilo. Kabla ya uteuzi huo Khamis alikuwa Meneja wa Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Wajumbe wengine wa BMZ ni Hamza Hassan Juma ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Kwamtipura kwa tiketi ya CCM na Suleiman Mahmoud Jabiri ambaye ni kocha wa mpira wa miguu na afisa wa juu wa Shirika la Kushughulikia Watoto Yatima, SOS
Wajumbe wengine ni Ally Saleh ambaye ni mshabiki mkubwa wa michezo na mwandishi wa habari wa BBC, Kombo Hassan Juma ambaye ni mkurugenzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na Amran Masoud Amran.

Katika mabadilko hayo, Waziri Shamuhuna amemng’oa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa ZFA Minyijuma Haji Saadati ambaye kwa taaluma ni mwalimu wa shule na kumrejesha Mzee Zam Ali aliyewahi kushikilia nafasi hiyo miaka ya nyuma.

Kabla ya kupewa wadhifa mpya, Zam alikuwa katibu katika Baraza la Michezo Zanzibar.

Tofauti na vyama vingine vya soka duniani, Waziri wa Michezo Zanziabr amepewa mamlaka ya kuteua Katibu Mtendaji wa ZFA wakati nafasi hiyo huwa ya kuchaguliwa na yeyote ana haki ya kugombea.

Mabadiliko hayo ya uongozi katika safu ya juu ya vyombo vikuu vya michezo Zanzibar yamekuja wiki chache kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa ZFA.

Wanamichezo wengi wa Zanziabr wanaamini kwamba mabadiliko hayo yana lengo la kuung’oa madarakani uongozi wote wa zamani wa ZFA uliopo chini ya Mwenyekti Ali Fereji Tamim na Makamu Mwenyekit Farouk Karim ambao inadaiwa wamechangia kuporomoka kwa soka la Zanzibar.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.