22 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Niko tayari kuwafundisha yosso - Chamangwana
 
2006-12-22 08:50:37
By  Jimmy Charles

Kocha mkuu wa timu ya Yanga, Mmalawi Jack Chamangwana, amesema kuwa japokuwa hajapewa taarifa ya kuzinoa timu za vijana wadogo lakini yuko tayari kufanya kazi hiyo kwa moyo mmoja.

Akizungumza na Nipashe jana, Chamangwana alisema kuwa uongozi wa klabu hiyo haujampa taarifa ya kuzifundisha timu za vijana za Yanga na zaidi ameona taarifa hiyo kupitia kwenye vyombo vya Habari.

”Sina taarifa na kazi ya kuwafundisha vijana,hadi sasa sijaambiwa lolote lakini niko tayari kuwafundisha vijana ni moja ya majukumu ya mwalimu hasa katika kukuza mchezo huo,”alisema Chamangwana.

Chamangwana alisema kuwa kazi hiyo itamuongezea sifa kubwa hapa nchini kwani atahakikisha jukumu hilo atakalopewa na viongozi wake analitimiza ipasavyo ili kuwaonyesha Watanzania uwezo wake katika kufundisha soka.

Alisema kuwa hakuna kazi nzuri kama ya kufundisha vijana ”ni kazi nzuri kwani itanisaidia sana kuonyesha uwezo wangu wa kufundisha,sina wasiwasi na hilo wakinipa taarifa nitakubali,” aliongeza Chamangwana.

Hivi karibuni uongozi wa klabu hiyo ulisema kuwa umemteua Chamangwana kuzifundisha timu za vijana wadogo wa timu hiyo ambao watashiriki kwenye michuano ya Copa Cocacola, itakayoshirikisha timu za vijana wadogo.

Kuteuliwa huko kwa Chamangwana aliyefanikisha kuipa ubingwa timu ya Yanga mara mbili mfululizo kuwa kocha wa vijana kumetokana na ujio wa makocha wawili kutoka Poland ambao watawasili kati ya Januari 6 na 7, mwakani.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.