22 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Uchaguzi Mkuu wa Yanga kuwa Feb.
 
2006-12-22 08:51:18
By  Jimmy Charles

Uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga unaosubiriwa kwa hamu na wanachama wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika mwezi Februari, mwakani.

Akiongea na Nipashe jana,aliyekuwa mwenyekiti wa kundi la Yanga asili, Yusuph Mzimba, ambaye kwa sasa ni mmoja wa wajumbe wa kuratibu zoezi zima la uchaguzi, alisema kuwa maandalizi ya uchaguzi huo tayari yameshaanza na sasa hivi wanakamilisha baadhi ya makubaliano.

Mzimba alisema kuwa kinachofanyika sasa hivi ni kukamilisha taratibu zote zilizokubaliwa na makundi yote na mara baada ya kukamilisha taratibu hizo wataanza rasmi zoezi la kutoa fomu.

”Uchaguzi wetu upo tutaufanya mwakani mwezi wa pili sasa hivi kuna baadhi ya mambo tunayakamilisha yakikamilika hayo kazi ya kuanza kutoa fomu itafanyika,”alisema Mzimba.

Mzimba alisema kuwa mambo yaliyobakia yatakamilika kabla ya mwaka huu kumalizika ili kutoa nafasi zaidi kwa kamati itakayoteuliwa kusimamia uchaguzi kuanza kazi yake mapema.

Aidha alisema kuwa katiba itakayotumika katika uchaguzi huo ni ya mwaka 1992 inayowalenga wanachama wenye kadi zinazotambulika na katiba hiyo.

Mzimba aliongeza kuwa mara baada ya kupata viongozi watakaokuwa madarakani kihalali, suala la kwanza ambalo watatakiwa kulishughulikia ni kukarabati kikamilifu jengo la klabu hiyo pamoja na kuhakikisha timu inafikia malengo watakayojiwekea.

Mara ya mwisho kwa klabu hiyo kufanya uchaguzi wake kwa kutumia katiba ya mwaka 1992 ilikuwa ni mwaka 1997,ambapo Agosti 23, 2003, klabu hiyo ilifanya uchaguzi wake kwa kutumia katiba ya kampuni.

Klabu ya Yanga inaongozwa na uongozi ulio chini ya Rais wake ,Francis Kifukwe,ambao ulifikia kikomo mwezi Agosti, mwaka huu baada ya kuchaguliwa kwenye uchaguzi uliofanyika Agosti 23,2003.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.