23 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Madaraka kuwa kocha msaidizi Simba
 
2006-12-23 08:27:44
By Somoe Ng’itu

Uongozi wa klabu ya Simba umemtangaza, Bakari Madaraka wa AFC ya Arusha kuwa kocha msaidizi wa timu yao, huku mfadhili mkuu wa sasa, Dionis Malinzi akiwa mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini.

Kocha huyo ambaye sasa yuko katika benchi la ufundi la timu ya mkoa wa Arusha ndiye pekee aliyekuwa msaidizi wa Mbrazil, Neider dos Santos huku wengine aliokataa kuwataja kukataa nafasi hiyo na kutaka kushika nafasi ya kocha mkuu.

Katibu mwenezi wa klabu hiyo, Said Rubeya ’Seyduo’ alisema pia kamati ya utendaji iliyokutana jana iliamua kuwateua Abu Wahab, Malinzi na Ally Sykes kuwa wajumbe wa baraza la wadhamini.

Aliwataja walioteuliwa kuwa walezi wa klabu hiyo kuwa ni Ally Hassan Hamis, John Lamba ’Magomamoto’ na Salum Pazi baada ya wengine wawili waliokuwepo, Ally Tambwe na Salehe Gurumu kufariki.

Alisema kuwa kocha huyo ataungana na kikosi cha wachezaji wa katika mazoezi yatakayoanza Desemba 28 na baadaye kuelekea visiwani kwenye mechi maalumu za sherehe ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitakazoanza Januari 8 baada ya kukubali mwaliko kutoka katika chama cha soka cha Zanzibar (ZFA).

Alisema wakiwa Zanzibar watacheza mechi ya kwanza na mabingwa wa Pemba, Mundu huku mshindi katika mchezo huo akikutana kati ya Miembeni au Malindi kwenye mchezo wa fainali.

Aliongeza kuwa mara baada ya sherehe hizo timu yao inatarajia kuweka kambi visiwani humo kujiandaa na mechi yake ya kwanza ya michuano ya kombe la shiriksho ambapo wamepangwa kuanza na Textile de Pungue ya Msumbiji.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.