23 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mziray ni muongo - Mwakalebela
 
2006-12-23 08:28:45
By Somoe Ng’itu

  Katibu mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela.  
   
Shirikisho la soka nchini (TFF) limesema kuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa na klabu za Simba na Yanga, Syllersaid Mziray anasema ’uongo’ kuhusiana na suala la maamuzi ya shirikisho hilo juu ya mchezaji, Athumani Iddi.

Akizungumza jana na Nipashe, katibu mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema kuwa anashangazwa na kocha huyo ambaye ni msomi ’kuudanganya’ umma kuwa Tanzania bado iko katika soka la ridhaa wakati inafahamika wazi kuwa sasa tumeondoka kwenye hatua hiyo.

Alisema kuwa Mziray ambaye ni mjumbe wa kamati ya maendeleo ya vijana ya TFF anaposema kuwa shirikisho limeboronga katika maamuzi hayo ni sawa na kujisema yeye mwenyewe kwa sababu kuundwa kwa kamati hiyo ni kielelezo cha kujiandaa kikamilifu kuingia katika soka la kulipwa.

”Namshangaa msomi kama Mziray anaposema kuwa Tanzania bado iko katika soka la ridhaa wakati anafahamu wazi kuwa wachezaji wanalipwa fedha nyingi wakati wa usajili, mishahara na pia wanasaini mikataba inayotambulika kisheria,” alisema Mwakalebela.

Aliongeza kuwa kocha huyo amekuwa akiuponda uteuzi wa wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars kwa kuwa na wachezaji wengi kutoka Simba na Yanga jambo ambalo hata yeye alikuwa analifanya alipokuwa mwalimu wa timu hiyo.

”Anashangaza sana kusema Stars imejaa wachezaji wa Simba na Yanga wakati yeye alipokuwa na timu hiyo, kikosi chake cha kwanza kiliwahi kuwa na wachezaji tisa kutoka Simba aliyokuwa akiifundisha na mmoja wa Yanga,” aliongeza.

Mziray alipokuwa katika mahojiano kwenye kipindi cha michezo cha redio one alisema kuwa TFF imeboronga suala la Athumani Iddi kwa sababu soka la Tanzania bado ni la ridhaa.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.