25 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ruzuku michezoni itatolewa kwa sababu maalum- Thadeo
 
2006-12-25 10:20:56
By George John

Baraza la Michezo la Taifa, BMT, limetoa ufafanuzi kuwa ruzuku kwa vyama vya michezo itakuwa ikitolewa kutokana na sababu maalum na si kugawa kiholela kwa vyama husika.

Katibu Mkuu wa BMT, Leonard Thadeo, alitoa ufafanuzi huo hivi karibuni wakati wa semina ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya michezo iliyoandaliwa na baraza hilo.

Alisema tayari baadhi ya vyama vimeshapatiwa ruzuku hiyo kulingana na matatizo yanayovikabili lakini akakiri kuwa si vyama vyote vya michezo vimepatiwa ruzuku hiyo.

Ufafanuzi huo wa Thadeo ulifuatia kilio cha muda mrefu cha vyama vya michezo nchini kuomba kupatiwa ruzuku toka serikalini kwa ajili ya kumudu gharama za lazima za uendeshaji wa shughuli za msingi za vyama husika kwa maendeleo ya michezo nchini.

Maombi hayo yanahusisha zaidi vyama vinavyoongoza michezo ya ridhaa ambayo haiingizi kipato cha aina yoyote kama ilivyo soka.

Katibu mkuu huyo alisema baadhi ya vyama (hakuvitaja) vimewezeshwa kulipa ada ya uanachama katika mashirikisho ya kimataifa na vingine kuendesha chaguzi baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa muda mrefu.

Wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Waziri Mohamed Seif Khatib alitaja fungu ambalo ni mahsusi kwa ajili ya kuvipatia ruzuku vyama kwa ajili ya kufanikisha shughuli zake.

Vyama vya michezo ya ridhaa, kwa muda mrefu vimekuwa na hali mbaya ya ukata na vingi kati ya hivyo havina hata ofisi za kuendeshea shughuli za michezo husika kitaifa na badala yake gharama za uendeshaji kuachwa kwa viongozi wa vyama.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.