25 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Yanga kuunda kampuni baada ya uchaguzi
 
2006-12-25 10:23:20
By Jimmy Charles

Klabu ya Yanga inatarajia kuunda kampuni ya umma itakayoshirikisha wapenzi na wanachama wa klabu hiyo mara baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Februari, mwakani.

Akiongea na Nipashe, aliyekuwa mwenyekiti wa kundi la Yanga asili, Yussuf Mzimba alisema kuwa kwa sasa wanapanga mikakati ya kuunda kampuni hiyo na mara baada ya kumaliza zoezi la uchaguzi watafanya usajili wa kampuni hiyo.

Alisema kuwa lengo lao ni kuunda kampuni ya umma itakayotoa fursa kwa kila mkereketwa wa klabu hiyo kuwekeza kwa kiasi chochote alichonacho ili kuiletea klabu hiyo mafanikio.

”Lengo letu ni kuhakikisha wanachama wote wa klabu ya Yanga wanaichangia klabu yao ili kuepuka migongano ya mara kwa mara,unajua kama mtu anakuwa na msaada na klabu hawezi kugombea visenti vya mlangoni wakati atakuwa anajua wazi kuwa kuna gawio atapata,”alisema Mzimba.

Mzimba alisema kuwa kwa sasa klabu hiyo haina kampuni ya aina yeyota na inajiendesha kama klabu na hata viongozi wanaoiongoza klabu hiyo wapo kwa ridhaa ya wanachama baada ya kukubaliana.

Alisema kuwa baada ya kuona ’longolongo’ zimekuwa nyingi waliamua kuvunja kampuni ya watu wachache na kukubaliana kuanzisha kampuni ya umma.

”Hatuwezi kuamuliwa jambo la watu 12,tumeivunjilia mbali kampuni hiyo na sasa hivi klabu pamoja na timu vinaendeshwa na wanachama wenyewe ambao kwa pamoja tumekubaliana kuwapa baadhi ya watu jukumu la kuiendesha klabu,”aliongeza Mzimba.

Aidha Mzimba alisema kuwa hali ni shwari ndani ya klabu hiyo na wanachoshughulikia sasa hivi ni suala zima la maandalizi ya michuano ya kimataifa na uchaguzi.

Alisisitiza kuwa zoezi la uchaguzi litakalofanyika mwezi Februari litawahusu wanachama wenye kadi za mwaka 1992 na kuwataka wanachama hao kulipia kadi zao ili kuwa na haki ya kupiga kura mara kitakapofika kipindi cha uchaguzi.

  • SOURCE: Nipashe
Comment on this article
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.