|
THI kutibu wagonjwa wa moyo kwa gharama nafuu
2006-12-28 10:05:29
Na Jackson Kalindimya
Taasisi ya Moyo nchini(THI) ambayo imeingia mkataba na taasisi iitwayo SES-Bonn ya Ujerumani kwa lengo la kuinua ubora wa utaalamu na vifaa ili kukifanya kituo hicho kuwa na hadhi ya kimataifa.Makala hii ya Mwandishi Wetu, Jackson Kalindimya yazungumzia mkakati huo.
Wakati magonjwa ya moyo yanaendelea kuongezeka katika nchi mbalimbali zinazoendelea ikiwemo Tanzania kutokana na kuiga mfumo wa maisha ya nchi za magharibi na sababu nyinginezo, ni muhimu sana mkazo mkubwa ukawekwa katika kubadili aina ya maisha ya watu, ikiwa pamoja na kutoa uzito mkubwa wa kuushughulikia ugonjwa huo, badala ya mkazo mkubwa kuwekwa kwa ugonjwa wa Ukimwi pekee kuwa ndio tishio kwa maisha ya watu.
Hatuwezi kutilia mkazo kuangalia kwa makini na nguvu nyingi kushughulikia tatizo la ugonjwa wa Ukimwi pekee ambako nguvu nyingi zinatumika.
Ni muhimu kwa magonjwa mengine kama ya moyo kupewa uzito mkubwa badala ya kuachiwa taasisi binafsi, mashirika yabebe dhamana hiyo kwa uzito mkubwaalisema Prof Gunter Hennersdorf wa taasisi iitwayo SEB-Bonn ya Ujerumani
Kwa muda mrefu sasa, serikali na watu binafsi wamekuwa wakitumia gharama kubwa kupeleka wagonjwa wa moyo kwenda kutibiwa nchi za nje kutokana na kutokuwepo kwa huduma bora ya aina hiyo hapa nchini ili kuyanusuru maisha ya wagonjwa.
Hali hii imekuwa ikisababisha wagonjwa wengi ambao hawana uwezo wa kwenda kujitibu wenyewe, kusubiri kupata bahati ya kusafirishwa na serikali kupitia Wizara ya Afya. Hata hivyo kutokana na gharama kubwa na wingi wa wagonjwa ni wachache tu wanaopata bahati hiyo.
Taasisi ya Moyo nchini(THI) katika kutambua hali halisi ilivyo, imekuwa ikijidhatiti kukusanya utaalamu na wataalamu wenye sifa za kutosha kumudu changamoto zilizopo ili kuyaokoa maisha ya watanzania wengi wanaougua ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mkuu wa THI, Dk Ferdinand Masau akizungumzia mikakati ya hospitali hiyo kuifanya kuwa bora zaidi kwa utoaji wa huduma ya tiba ya moyo na upasuaji nchini, alisema hivi karibuni imeingia mkataba na taasisi binafsi ya Ujerumani iitwayo SEB ambayo itakuwa ikitoa watalamu wake katika fani mbalimbali za tiba za moyo kufanya kazi hapa nchini katika hospitali hiyo na kutoa fursa kwa watalamu waliopo katika hospitali hiyo kwenda kuongeza ujuzi nchini Ujerumani.
Lengo hasa ni kuifanya THI kuwa kituo cha moyo cha kimataifa ambacho kinajitosheleza kwa utaalamu,wataalamu na vifaa vya hali ya juu kama ilivyo kwa hospitali nyingine za aina hiyo duniani.
Alitoa ufafanuzi huo mbele ya Prof. Gunter Hennersdorf (Consultant Cardiologist), Sr Elizabeth Fichtner (Senior Nursing Officer), Dk Horst Vick (Consultant Nephrologist), na M.Schweitzer (Consult Biomegical Engineer) waliofika nchini kwa ajili ya kukamilisha utaratibu huo.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo ni kwamba taasisi hiyo ya Ujerumani itakuwa ikituma wataalamu wake kuja nchini kutoa mafunzo kwa madaktari na wataalamu wa kitanzania ikiwa pamoja na baadhi ya madaktari hao kwenda nchini Ujerumani kuongezea utalaamu zaidi ili wamudu kwa ufanisi changamoto mbalimbali za tiba.
THI tangu ianzishwe mwaka 2002 hadi sasa, tayari imetibu wagonjwa wa moyo wapatao 110.Gharama za tiba ya moyo kwa magonjwa ya kawaida ni kati ya dola 3,000 au zaidi ya 15,000 kutegemea na aina ya ugonjwa na kiwango chake cha uambukizo.
Gharama zinalazimika kuwa kubwa duniani kote kutokana na matumizi ya vifaa vya hali ya juu ikiwa pamoja na utalaamu wake ili kumudu tiba za ugonjwa huo hali ambayo inafanya kuwa sio rahisi mgonjwa kutibiwa bure zaidi ya kutegemea ufadhili wa watu, taasisi,mifuko,mashirika,harambee za kuhamasisha michango na kampuni mbalimbali zinazobeba gharama za tiba kwa lengo la kuyanusuru maisha ya wagonjwa.
Dk Masau alisema katika kujaribu kukabiliana na gharama za uendeshaji wa kituo hicho na kutibu wagonjwa wengi zaidi, wamepeleka maombi serikalini ili kuwe na utaratibu wa wagonjwa wanaosubiri kwenda kutibiwa katika nchi za Ulaya na India, wapelekwe kutibiwa katika hospitali hiyo kwa gharama nafuu zitakazolipwa na serikali, ikilinganishwa na gharama za usafiri wa kwenda na kurudi toka nchi za Ulaya na India zinazoendelea kubebwa na serikali na watu binafsi.
Watu wetu wengi ni masikini hawawezi kumudu gaharama kubwa ndio maana tumeiomba serikali iangalie uwezekano wa kutumia fursa zilizopo hapa THI.
Hata hivyo maombi yetu yanashughulikiwa taratibu licha ya kuwa tuna matumaini kuwa yatapewa uzito unaostahili siku moja.Gharama za tiba zitapangwa kwa ushirikiano na watalaamu wa serikali kwa kuchambua hali halisi na kuzingatia gharama nafuu zisizoathiri ubora wa tiba ambazo zinafaa kutumiwa kumudu tiba za wagonjwa alisema Dk Masau.
Prof Hennersdorf alisema kwa kushirikiana na THI kutainua ubora wa huduma za upasuaji mkubwa wa moyo, vifaa mbalimbali vya tiba ambavyo gharama zake ni kubwa, huduma kwa wagonjwa na mafunzo kwa wataalamu mbalimbali watakaofanya kazi katika mazingira bora yatakayoboreshwa katika kituo hicho.
Kuhusu uutoaji wa huduma za aina hiyo nchini Ujerumani ikiwa pamoja na kuwafikia watu wa hali zote, Prof Hennesdolf alisema kuwa nchini kwao kuna mfumo wa bima ya afya ambapo kila mwanachama anakuwa na fursa kutibiwa katika hospitali mbalimbali ambapo ni watu wachache tu wasio wanachama ndio wanaolazimika kugharamia matibabu hayo.
Dk Masau alituomba ushirikiano ndio maana tumeonyesha nia ya kusaidia kwa vitendo alisema.
Miongoni mwa sababu zinazochangia kusababisha kuongezeka kwa wagonjwa wa moyo kwa mujibu wa Prof Hennersdorf ni mfumo wa maisha ya zama hizi nchini ikiwa pamoja na nchi nyingine zinazoendelea duniani.
Uhamaji wa watu kutoka vijijini kwenda mijini na kuachana na maisha ya asili ambayo yanaruhusu ukuaji wa mwili kwa njia za asili, hali ya vyakula vya zama hizi, kuibuka kwa magonjwa ya kisukari, umasikini na matatizo mengineyo.
Kimsingi serikali na jamii kwa ujumla, zina changamoto kubwa ya kuhakikisha zinatumia kikamilifu fursa zilizopo za kutibu wagonjwa wa moyo zinazopatikana katika hospitali hiyo ili kunusuru gharama kubwa zinazotumika kusafirisha wagonjwa hao kwenda kutibiwa nchi za nje.
Gharama za tiba za moyo ni kubwa na hivyo ni vyema
SES-Bonn Germany imekuwa ikiisaidia THI tangu mwaka 2003 kwa kuleta wataalamu waandamizi katika taasisi katika kubuni hospitali itakavyokuwa, kutoa mafunzo na kuanzisha wovuti yao ambapo sasa wanashiriki kuanzisha kituo cha kimataifa cha moyo ambapo Prof Hennersdorf ndiye mwakailishi na mratibu wa ushirikiano kati ya taasisi ya moyo ya Ujerumani(Germany Heart Centre Voelkkinggen na THI.
Pia mipango inaendelea kushirikiana na setikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya,hospitali na taaisi nyingine zinazoonyesha kuhitaji ushirikiano ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na kituo maalum.
|