|
Siku ya Mtoto Afrika:Usafirishaji watoto haramu udhibitiwe
2007-06-16 09:28:11
Na Mwandishi Wetu
Wakati leo ni Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo inaadhimishwa duniani kote, Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kitaifa yatakayofanyika mjini Dodoma.
Tarehe hii ni kumbukumbu ya mauaji yaliyotokea Soweto Afrika Kusini ambapo yalifanyika maandamo ya kudai haki kwa watoto.
Wakati imetimia miaka 31 sasa, tangu maelfu ya wanafunzi weusi wa shule za Afrika Kusini waliandamana katika mitaa ya Soweto mnano Juni 16, 1976 ili kupinga elimu duni wanayofundishwa na kudai haki ya kufundishwa kwa lugha yao bado kuna matatizo mabli mbali yanayomkabili mtoto wa Afrika.
Hatua ya wanafunzi hao, iliamsha hasira za makaburu ambapo mamia miongoni mwao walipigwa risasi na katika wiki mbili za kupinga tukio hilo, kulikuwa na ongezeko la watu 100 kuuawa na zaidi ya elfu moja kujeruhiwa.
Katika siku hiyo, wanafunzi weusi na watoto wa shule walikusanyika ili kupinga serikali ya kibaguzi kuwadhalilisha weusi katika masomo wakitakiwa kujifunza kwa kutumia lugha ya Afrikaans, ambayo ni ya wazungu wachache nchini humo.
Tukio hilo liliamsha msuguano mkubwa, ambapo polisi walitumia nguvu, baada ya kupokea maagizo toka serikalini kwamba wadhibiti nyendo hizo kwa gharama yoyote ile na kujikuta wakifyatua risasi,na kuua zaidi ya watu 500 na kujeruhi watu 1,000.
Tangu hapo, siku hiyo imekuwa ikiadhimishwa kwa kufanya shughuli hizi na zile kuonyesha hali fulani.
Licha ya maadhimisho ya tukio hilo la kihisitoria, imekuwa muhimu kukumbushana kuhusu hali ya watoto hasa wale walio katika mazingira magumu.
Hii pia imekuwa ikielekeza kufikiria kwa kina kuhusu matatizo maalum na kuchukua hatua muafaka ili kuhakikisha kuwa hatua muafaka zinachukuliwa kwa kila mtoto.
Kwa ajili ya kumbukumbu ya tukio hilo la aina yake kwa wale waliouawa na walioandamana.
Siku ya Mtoto wa Afrika, imekuwa ikiadhimishwa duniani kote katika tarehe 16 June ya kila mwaka tangu mwaka 1991 ambapo ilianza kuadhimishwa mara ya kwanza na Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU).
Hapa nchini,Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, yanayotarajiwa kufanyika kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dodoma,William Lukuvi, alisema mkoa pia umeandaa shughuli mbalimbali maalum kwa ajili ya siku hiyo.
Miongoni mwa shughuli hizo zilizondaliwa na Halmashauri ya Watoto mkoani itafanya sherehe fupi katika Shule ya Sekondari Msalato ambapo kitabu kuhusu uangalizi wa watoto kitazinduliwa katika Uwanja wa Dodoma.
Pia kutakuwa na maonyesho ya watoto wenye vipaji maalum katika kazi za sayansi na sanaa ikiwa pamoja na vyakula vyenye lishe.
Kufuatia azimio la OAU, Siku hiyo imekuwa ikitumiwa kama fursa ya kuonyeha maendeleo ya hali halisi kuhusu afya, elimu,usawa na ulinzi kwa watoto wote wa kiafrika.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni `Usafirishaji wa Watoto`
Yawezekana ikawa vigumu kupata takwimu sahihi kuhusu watoto waathirika wanaosafirishwa toka kwao kitaifa, kikanda au kidunia.
Kwa mujibu wa taasisi iitwayo Plan inayoshughulikia ushirikiano wa kuwajali watoto iliyoanzishwa mwaka 1937 kwa ajili ya kuleta matumaini na kuwasaidia watoto masikini zaidi duniani, usafirishaji wa watoto ni moja ya udhalilishaji wa haki za binadamu katika dunia ya sasa ambayo inahususisha mamilioni ya watoto duniani kote.
Inahusisha usafrishahi haramu wa binadanmu,hasa wanawake na watoto kwa dhamira ya kuwauza au kuwadhalilisha katika ajira.Shirika la Kazi Duniani (ILO) linasema kuwa
`Ajira kwa waoto ni tatizo kubwa,ambayo inaathiri mmtoto mmoja kati ya watoto sita katika dunia ya sasa`
Katika ripoti yenye kurasa 79 kuhusu hali halisi ya usafrisghaji watoto nchini Togo iliyotolewa mwaka 2003, kama mfano wa usafirishaji huo katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Imeonyesha jinsi gani watoto, wakiwemo wale wachanga wanaofikia umri wa miaka mitatu wanavyodhalilishwa kwa kazi za nyumbani na kilimo katika nchi mbalimbali.
Wasafirishaji hao, wamekuwa wakiwaondoa watoto nyumbani kwa ahadi ya kuwapeleka kwenye shule zenye ubora wa hali ya juu na vyuo vya ufundi katika nchi za nje.
Watoto wengi miongoni mwao ni yatima, ambao hulazimishwa kuwa watafutaji wa ‘mkate’ wa maisha yao, baada ya wazazi wao kufa kwa ugonjwa wa Ukimwi au sababu nyingine.
Kashafa kuhusu ajira ya watoto katika Afrika Magharibi iliibuka mwaka 2002,ambapo karibu nusu ya wazalishaji wa chokoleti nchini Marekani walihusishwa na uvunaji wa kokoa ulioanywa na watoto wadogo toka katika nchi ya Côte d’Ivoire.
Watoto wengi miongoni mwao walikuwa wamesafirishwa toka katika nchi jirani kama vile Mali na Burikina Faso.
Hali hii ndiyo iliyosababnisha Joseph Addison aainishe.
`Elimu ni mwenza ambaye hakuna hali yoyote ile inayoweza kuishusha, hakuna jinai inayoweza kuisambaratisha, na hakuna adui anayeweza kuivujavunja au kuifanya mateka.
Nyumbani,rafiki, nchi za nje ni utambulisho na katika jamii ni hazina.Ina thamani ya pekee.Bila ya hiyo je mtu anakuwa na thamani gani?
Ni mtumwa na uwezo wake kwa kuchambua mambo unakuwa ni mdogo` alisema.
Wastani wa watoto wa Kiafrika umebaki kuwa katika kifungo cha umasikini ambacho ni kiini kwa ajili ya kukosa elimu na kiini cha umasikini.
Kwa hiyo, umasikini umekuwa ukirithishwa toka kizazi kimoja kwenda kingine.
Maazimioo na mikataba ya kimataifa, ikiwemo ile ya the International Covenant on Economic, Social and Cultural Rights (ICESCR) - Article 13 na the African Charter on the Rights and Welfare of the Child (ACWRC) - Article 11 inatambua kuwa elimu ni haki ya msingi kwa kila mtoto.
Kila taifa pia linatambua umuhimu wa elimu kwa ajili ya maisha, na kwa hiyo kila taifa.
Kuonyesha dhamira ya kuhakikisha kuwa kila raia wake anafanikisha azma hiyo ni suala jingine.
Kwa mujibu wa Plan, moja ya njia muhimu kabisa ya kudhibiti au kuzuia usafrishaji wa watoto ni vijana kuwapa fursa ya kupata elimu bora.
Kwa kadri vijana(na watu wazima) wanavyotambua kuhusu haki zao, ndivyo wanavyopata fursa ya kukabiliana na unyanyasaji wa haki hizo.
Kwa kuonyesha dhamira hiyo, kila mzazi na watoto wanahitaji kila mtoto kuwa na uwezo wa kuisoma na kuandika ikiwezekana kupata elimu bora.Lakini sio kila mtoto ana uwezo wa kuipata.
|