|
Ongezeko la joto duniani laathiri ndege wahamaji
2007-08-23 10:35:10
Na
Mwenendo wa makundi ya ndege na wanyama ambao wamekuwa wakihama toka sehemu fulani ya dunia kwenda eneo jingine katika majira fulani ya mwaka, yameathiriwa na ongezeko la joto duniani linaloikabili dunia kwa sasa.Makala hii kwa msaada wa mtandao yafafanua.
Kuyeyuka kwa barafu katika ncha za kaskazini na kusini, kupanuka kwa jangwa na athari za joto baharini ni miongoni mwa tishio dhahiri ilinalojitokeza kwa sasa duniani hata kuathiri ndege na wanyama wanaohamahama kwa mujibu wa ripoti ya EU kuhusu hifadhi ya mazingira asili iliyotayarishwa kwa udhamini wa Serikali ya Uingereza.
Ripoti hiyo imezinduliwa katika kikao kilichowahusisha wakuu wa mazingira ya asili katika Umoja wa Ulaya huko Scotland.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,ongezeko la joto duniani, tayari limeathiri mwenendo wa misafara ya baadhi ya ndege wahamiaji na wanyama.
Idara ya Mazingira,Chakula na masuala ya vijijini(Defra) ya Uingereza ndiyo iliyoepwa dhamana y kufanya utafiti ambayo iliongozwa na the British Trust for Ornithology.
Mkutano huo uliitishwa, ili kujadili njia za kuwasaidia wanyamapori kukabiliana na ongezeko la joto duniani.
Mabadiliko ya nyakati.
Wanasayansi tayari wameanza kuchunguza mabadiliko makubwa kuhusu mfumo wa uhamaji wa ndege, samaki na wanyama, ikiwa njia ya kukabiliana na hali ya joto ambayo tayari imeanza kushika kasi.
Baadhi ya viumbe ambavyo vimekuwa vikihusishwa na nchi za kusini kama vile the little egret, the loggerhead turtle, na the red mullet, wamekuwa wakiongezeka sana katika kuzunguka Uingereza hali ambayo ilikuwa tofauti kwa miaka iliyopita.
Ndege aina ya Krill, kutokana na mfumo wao wa chakula, nao wamekuwa wakiathiriwa sana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ndege wengine aina ya Wading nao wamekuwa wakitumia majira ya masika katika eneo la mashariki ya pwani ya Uingereza na wengineo chiff-chaffs wamakuwa wakibakia nchini Uingereza kwa mwaka mzima badala ya utaratibu wao wa kuhama kwenda eneo la kusini.
Wakati ambapo viumbe wengine wamekuwa wakijaribu kuchukuana na hali mpya iliyopo na kuelekea katika maeneo mbalimbali,utafiti umetahadharisha kuwa, hali hiyo haipo kwa wanyama wengineo ambao mazingira yao yakiharibika ni kwamba huanza kutoweka taratibu kutokana na kuyeyuka kwa barafu huko Arctic .
Hata mabadiliko kidogo ya joto baharini, yanaweza kuwa na athari kwa wanyama na kuathiri mfumo wao wa chakula baharini na hali nyingine.
Hii inafikiriwa kuwa, imechangia kuhusu kuporomoka kwa kasi katika mfumo wa chakula kwa baadhi ya ndege wa huko Scottland ambapo chakula walichokuwa wanakitegemea cha samaki kimekuwa adimu na kutishia uwepo wao.
Baadhi ya matishio ambayo yamekuwa yakitokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yamebainishwa katika utafiti huo kuwa ni:-
• Ongezeko la vimbunga ambavyo vinaathiri sehemu ya mazalia na mfumo wa chakula ikiwa pamoja na mitiririko wa samaki
• Kiwango cha usawa wa bahari kupanda juu, hata kuathiri pwani ambako ni makazi na mazalia ya viumbe hai wakiwemo kasa na wengineo.Karibu robo ya pwani zinazotumiwa na kasa katika eneo la Carribean yaweza kupotezwa katika karne hii, ambapo viumbe wa baharini na ndege wako katika hatari ya kusambaratishwa makazi yao.
• Ongezeko la joto baharini, laweza kuathiri mfumo wa uzalianaji wa viumbe, kwa sababu joto la maji kwa namna fulani litaathiri jinsi zao.
• Ongezeko la uhaba wa maji katika kanda nyingi, laweza kuathiri sehemu mbalimbali ambayo ni makazi ya viumbe wanaoishi kwa kutegemea maji katika maeneo hayo.
• Kupanuka kwa jangwa la Sahara, kunaweza kuwaathiri ndege na wanyama wanaofanya safari za masafa marefu, ambao walikuwa na kawaida ya kupumzika katika maeneo yenye neema ili kukusanya nguvu upya na kuendelea na misafara yao. Sasa mambo yanakuwa magumu.
``Mabadiliko ya hali ya hewa tayari yanaathiri mfumo wa viumbe wanaohamahama`` anasema Humphrey Crick kutoka British Trust for Ornithology, ambako mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo anatoka.
``Kutoka katika maeneo ya kaskazini ya Sahara hadi bahari za kusini zinaonyesha kuwa athari kwa kiasi kikubwa zinaongezeka.
``Kuna njia za kuwasaidia viumbe, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini tunahitaji kupata suluhisho la kidunia kuwasaidia wanyama ambao wanaogelea,kuruka na kusafiri maelfu ya maili kila mwaka``.
Mfumo wa asili, umekuwa na kawaida ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hata hivyo, kwa hali ya sasa imekuwa ni changamoto kubwa katika mfumo huu, ambao unazalisha hali isiyotarajiwa katika uso wa dunia na majini.
Hata hivyo, hofu ipo kwamba mabadiliko ya sasa,ambayo yamekuwa ya kasi sana kwa viumbe kuchukuana vyema na hali hiyo, na kuhitajika mikakati mipya ya kukabiliana nayo ili kuweza kuishi.
Hali hii imekuwa ikikabiliwa na kuharibiwa kwa mfumo wa asili wa mazingira ikiwemo ukaushaji wa maeneo nyevunyevu,ukataji wa misitu na maendeleo ya ukanda wa pwani- na kwamba kama tabia hiyo itaendelea kuathiriwa na joto duniani ni kwamba kimsingi hakuna sehemu ya kukimbilia.
Ripoti hiyo ina ujumbe muhimu kwa maofiusa wa hifadhi ya mazingira walokutanika huko Scotland ulioandaliwa na Defra.
Walikubaliana kuchukua hatua muhimu za ‘kibailojia’ ili kupanua wigo wa kumudu viumbe wanaohamahama wakati mabadiliko ya mazingira yakishika kasi.
Mikakati yote ya hifadhi ya mazingira yatakiwa kuchukuliwa hatua madhubuti na kulindwa kulingana na asili, vinginevyo itakuwa na maana ndogo kwa wanyama ambao sehemu zao za mazalia zakabiliwa na tishio na hawana sehemu nyingine ya kuhamia.
Mabadiliko ya chakula kwa ndege wa baharini yamekuwa yakiwaathiri sana na kuwapotezea ule uwezo, ikiwa pamoja na kuwapunguzia fursa za kuishi na kuzaliana kwa mujibu wa utafiti mpya.
Wanasayansi wamefanya majaribio katika maabara kuhusu mfumo wa chakula kwa ndege aina ya kittiwakes katika bahari ya Bering - mabadililko yaliyosababishwa na ongezeko la joto duniani.
Taarifa ya RSPB inasema kuwa, mabadiliko ya chakula cha ndege wa baharini yaweza kuwa na athari mbaya kuhusu uwezekano wao wa kuendelea kuishi.
Miaka ya 1980 ilianza kushuhudia kuporomoka kwa idadi ya ndege wenye miguu myekundu kittiwakes katika kisiwa cha Pribilof huko kusini-mashariki ya bahari ya Bering Sea,katika pwani ya Alaska.
Idadi hiyo imekuwa ikiporomoka sana katika kipindi cha miongo miwili.
Sababu haiko dhahiri, licha ya kuwa wanasayansi wanasema kuwa mabadiliko ya mfumo wa chakula ambayo yamekuwa yakijitokeza katika nyakati fulani.
|