26 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wasso, Odhiambo hawakuwa na vibali - Uhamiaji
 
2008-03-26 08:42:23
By Onesmo Kapinga

Idara ya Uhamiaji imesema kuwa wachezaji wawili wa klabu ya soka ya Simba Ramadhani Wasso na Moses Odhiambo walizuiliwa kuingia nchini Nigeria kutokana na hawakuwa na vibali vya kufanyia kazi nchini.

Wachezaji hao walirudishwa na Idara ya Uhamiaji ya Nigeria ambako walikwenda kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa raundi ya pili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Enyimba ya nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, msemaji wa idara hiyo, Abdi IjImbo alisema kuwa uongozi wa Simba ulikuwa haujalipia gharama za kibali hicho.

Ijimbo alisema kuwa Wasso alikuwa na kibali alichoombewa na watani wao wa jadi Yanga na kutokana na sheria za idara hiyo, Simba walitakiwa kwenda kumwombea kingine. Odhiambo alikuwa na kibali cha Moro United.

Ijimbo wao alidai Uhamiaji haikuwa na taarifa ya maandishi kuhusu kuvunjika `ndoa` ya wachezaji na timu zao za zamani.

Alisema kuwa Simba kama walitakiwa kuvitumia vibali hiyo walitakiwa kuijulisha idara hivyo kitu ambacho hakikufanyika.

``Simba walileta maombi ya kutaka vibali vya kufanyia kazi kwa ajili ya wachezaji hao lakini walishindwa kuleta fedha mapema,`` alifafanua Ijimbo.

Alisema kuwa uongozi wa Simba ulizembea kuwalipia wachezaji hao Dola 1240 za Kimarekani ili waweze kupatiwa vibali hivyo.

Hata hivyo, wachezaji hao jana walipatiwa vibali vya kudumu vya miaka miwili baada ya uongozi wa klabu hiyo kwenda kuwalipia kiasi cha Dola 620 kila mmoja.

Wakati huo huo, makocha watatu wa klabu ya soka ya Yanga pia wamepatiwa vibali vya kufanyia kazi nchini.

Makocha hao ni Waserbia Dusan Kondic, Spasso Skolosviki na Srdjan Vojnon na pia Kocha wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.