26 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Stars kulipa kisasi kwa Msumbiji leo?
 
2008-03-26 08:43:41
By Somoe Ng\'itu

Timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars leo inatarajia kucheza na timu ya taifa ya Msumbiji, Black Mambas katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo ambayo inachezwa katika siku iliyopo katika kalenda ya Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA)kwa nchi mbalimbali kucheza mechi za kirafiki ni maalumu kwa Stars kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Harambee Stars ya Kenya.

Pia mchezo huo utakuwa nafasi kwa Stars kulipa kisasi kwa kuifunga ili kupunguza machungu ya mwaka jana wakati Msumbiji ilipoikatili ndoto ya Stars ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kupata ushindi wa 1-0, jijini, Dar es Salaam.

Akizungumza jana, kocha mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo alisema kuwa mechi hiyo ni kubwa na itakuwa ngumu kwa sababu wapinzani wao wameleta kikosi imara.

Maximo alisema kuwa Msumbiji ambao walitufunga katika mechi ya mwisho ya kuwania kufuzu kwenda kwenye fainali zilizopita za mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika na itakuwa na kazi ya kudhihirisha kuwa ushindi wao uliopita haukuwa wa kubahatisha.

Aliwataka Watanzania kuacha ushabiki wa klabu na kuungana pamoja leo kuishangilia Stars ambayo inahitaji ushirikiano wakati wote.

``Nawaomba watu waje wamevaa tshirt zenye rangi ya bluu na kupeperusha bendera ya nchi, tuachane na ushabiki wa klabu kwa sababu kila mmoja ni Mtanzania,`` alisema Maximo.

Naye nahodha msaidizi wa timu hiyo, Nadir `Cannavaro` Haroub aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kuwashangilia kwenye mechi hiyo na kuahidi kuwa watahakikisha ushindi unapatikana.

Mwamuzi wa kati wa mchezo huo atakuwa Oden Mbaga atakayesaidiana na Hamisi Chang`walu na Mpenzu.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.