27 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mvua yazizuia Stars, Msumbiji kucheza
 
2008-03-27 08:27:09
By Somoe Ng\'itu

Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, jana ilishindwa kucheza mechi yake ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya Msumbiji, Black Mambas kwenye Uwanja wa Taifa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha sehemu mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam.

Mvua hiyo iliyoanza saa sita mchana iliendelea hadi saa 11 jioni na kusababisha sehemu ya kuchezea ya uwanja huo, ambayo hivi sasa ina nyasi bandia kujaa maji na kushindikana mchezo huo kufanyika na timu zote mbili kurejea kambini.

Baada ya hali hiyo kutokea, timu ya Msumbiji iliombwa kukubali mchezo huo kufanyika leo lakini maafisa wa timu hiyo walikataa kutokana na wachezaji wake wa kulipwa kuhitajika katika klabu zao.

Taarifa ziliendelea kusema kuwa mechi hiyo itafanyika siku nyingine ambayo pia itakuwa katika kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Soka, FIFA.

Stars ilikuwa inataka kucheza mchezo huo kujiandaa na mechi yake ya keshokutwa dhidi ya Harambee Stars ambayo ni ya kwanza katika mashindano mapya ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambalo ni maalumu kwa wachezaji wa nyumbani.

Hii ni mara ya pili kwa Stars kupata `mshikemshike` wa kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa baada ya timu ya Angola kutofika katika muda uliopangwa na kusababisha vurugu kubwa kwa mashabiki wa soka hapa nchini.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.