|
Kipigo chaigawa Simba
2008-03-27 08:28:13
By Mwandishi Wetu
Kampuni ya bia ya Tanzania, TBL, inatazamiwa kudhamini michuano ya mwaka huu ya Kombe la Taifa itakayofanyika Mei, jijini, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo, kiasi cha Sh. milioni 580 kinatazamiwa kutumika kwa ajili ya zawadi, maandalizi, utawala na huduma za kufanikisha mashindano hayo.
Bingwa wa mashindano hayo anatazamiwa kujipatia sh. milioni 30, mshindi wa pili sh. milioni 15, mshindi wa tatu sh. milioni 7.5 na mshindi wa nne Sh. milioni tano.
Pia mchezaji bora, mfungaji bora, kocha bora na mwamuzi bora kila mmoja anatazamiwa kupatiwa kitita cha sh. milioni mbili.
Fedha zilizotengwa kwa ajili ya maandalizi ni pamoja na kugharamia usafiri wa kuja Dar es Salaam na kurudi, usafiri wa timu, jijini na pia malazi.
Gharama za utawala zitajumuisha uendeshaji wa mashindano, semina kwa waandishi wa habari na matangazo kupitia katika vyombo vya habari na mabao ya matangazo.
Taarifa ya TBL ilieleza kuwa mashindano hayo yatahusisha mikoa 23 kufuatia kugawanya kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Sasa wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke kila moja kupewa fursa ya kuingia timu badala ya ile ya kombaini.
TBL imeamua kujitosa kudhamini mashindano hayo ili kufufua mapenzi ya soka ya kimkoa, kuongeza ushindani, kuinua kiwango cha soka cha kitaifa na kuibua vipaji mikoani.
Katika michuano ya mwaka jana, timu ya mkoa wa Mbeya ndio iliweza kunyakua Kombe hilo.
|