25 Apr 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Simba yasamehe waliosimamishwa
 
2008-04-25 09:28:46
By Somoe Ng\'itu

Wachezaji wa Simba sita ambao walisimamishwa wiki iliyopita na uongozi wamesamehewa na leo wanatarajia kujiunga na wenzao kambini kujiandaa na mchezo wao wa marudiano na Yanga, ambao umepangwa kufanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini, Dar es Salaam.

Wachezaji hao waliosimamishwa ambao wamo katika kikosi cha kwanza ni pamoja na Athumani Machupa, Yahaya Akilimali, Victor Costa, Erick Majaliwa, Saidi Sued na Nurdin Bakari.

Akizungumza na Nipashe jana, mmoja wa viongozi wa Simba, ambaye alikataa kutajwa jina lake alisema kuwa wachezaji hao wamesamehewa kutokana na kuhitajika katika mchezo wa Jumapili, ambapo wanahitaji ushindi ili kujihakikishia ushiriki wao katika mashindano ya kimataifa mwakani.

Kiongozi huyo alisema kuwa kabla ya kuwapa taarifa za kuwasamehe wachezaji hao watatakiwa kujieleza mbele ya viongozi wa kamati ya utendaji na kuwasikiliza utetezi wao.

``Tutawasamehe wote, si unajua tunataka kuwafunga Yanga, ni lazima wote tuwe kitu kimoja ili kupata ushindi,`` alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa Simba itaendelea kutoa adhabu kwa wachezaji wake wote, ambao watakuwa wanafanya makosa bila kujali uwezo wa mchezaji husika ili kuijenga Simba yenye nidhamu.

Alisema pia maandalizi ya mechi yao ya keshokutwa yanaendelea vizuri na wanaamini kuwa watani zao hawataweza kufurukuta katika mchezo huo.

``Kuwafunga Yanga kwetu ni jambo la kawaida, kama vile kifo kwa binadamu,`` alitamba kiongozi huyo.

Wachezaji hao walisimamishwa kwa utovu wa nidhamu, ambapo walidaiwa kuwa walikuwa wakiwashawishi wenzao kugomea mechi ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Enyimba na pia kutishia kuhujumu mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliokuwa unawakutanisha na Toto Africans ya Mwanza.

Wakati huo huo, viingilio katika mechi ya keshokutwa, ambapo Simba atakuwa mwenyeji wa Yanga Sh. 20,000 kwa viti maalumu, Sh. 15,000 jukwaa kuu, Sh. 8,000 jukwaa la kijani na eneo la mzunguko ni Sh. 3,000.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.