09 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wanafunzi 38 Chuo Kikuu Dar waachiwa huru
 
2008-05-09 09:00:00
Na Hellen Mwango

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana iliwafutia mashtaka wanafunzi 38 wa Chuo Kikuu baada ya upande wa mashtaka kuona hawana nia tena ya kuendelea na kesi.

Kesi hiyo ilifutwa mbele ya Hakimu Mkazi Said Msuya, wa Mahakama hiyo.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Kenyella, aliomba mahakama kuwafutia washtakiwa mashtaka yao kwa kuwa upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea kuwashtaki tena.

Alidai kuwa, anaomba Mahakama kuondoa shauri linalowakabili wanafunzi hao.

Hakimu Msuya alisema kutokana na upande wa mashtaka kuona kuwa hauna nia ya kuendelea kuwashtaki wasomi hao, Mahakama haina sababu ya kupinga ombi hilo hivyo washtakiwa wote wameachiwa huru.

``Haya wasomi, upande wa Jamhuri umewaachia huru kwa hiyo vijana mkasome salama,`` alisema Hakimu Msuya.

Mapema mwezi uliopita, wanafunzi hao walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashtaka ya kufanya fujo.

Ilidai kuwa, Aprili 22, mwaka huu, eneo la Chuo Kikuu washtakiwa wote kwa pamoja, walikula njama ya kutenda kosa la kuwafanyia fujo wanafunzi wa wahadhiri wa chuo hicho.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa, washtakiwa hao pia, Aprili 22, mwaka huu, eneo la chuo hicho walifanya fujo na kusababisha wanafunzi wenzao kushindwa kusoma na wahadhiri kushindwa kufanya kazi zao.

Ilidaiwa kuwa, kitendo hicho kilisababisha usumbufu na shughuli za masomo kusimama hivyo kuwaathiri wanafunzi wenzao.

  • SOURCE: Nipashe
Tuma Maoni Yako
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.