09 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Magufuli ashiriki zoezi la kuteketeza zana...
 
2008-05-09 09:03:12
Na George Ramadhan, PST Mwanza

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Bw. John Magufuli juzi aliongoza zoezi la kuteketeza lundo la zana haramu za uvuvi ambazo zilikamatwa katika maeneo mbalimbali mkoani Mwanza.

Zoezi la kuteketeza zana hizo, lilifanyika katika dampo la Buhongwa, nje kidogo ya jiji la Mwanza na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. James Msekela, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Kanali (mstaafu) Peter Madaha na Mkurugenzi wa Uvuvi, Bw. Geofrey Nanyaro.

Akizungumza kabla ya kuteketeza zana hizo, Waziri Magufuli alisema kwamba serikali haiwezi kuvumilia uvuvi haramu kwa sababu madhara yake ni makubwa kwa uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.

Alisema uvuvi haramu umechangia kupungua kwa samaki ndani ya Ziwa Victoria kutoka tani 750,000 mwaka 2006 hadi tani 375,000 mwaka huu.

\"Hivi tunavyozungumza samaki wamepungua sana ndani ya Ziwa Victoria kutokana na uvuvi haramu ambapo kabla ya mwaka 2006 kulikuwa na mabilioni ya tani za samaki lakini sasa wamepungua hadi kufikia tani 375,000.

Aliongeza kwamba ili kukomesha uvuvi haramu, Serikali itafanya misako ya kushtukiza katika maduka yanayouza vifaa vya uvuvi ili kubaini wale wanaouza zana ambazo zimepigwa marufuku.

Aidha alisema kwamba Serikali pia itaweka Maofisa Uvuvi katika mipaka ili kuwakamata wale wanaosafirisha samaki wachanga kwenda nchi jirani.

Waziri Magufuli aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya, miji, manispaa na jiji kote nchini kushiriki katika kukomesha uvuvi haramu.

``Wakurugenzi wasikalie kukusanya tu ushuru wa samaki, lazima nao washiriki kikamilifu katika kukomesha uvuvi haramu`` alisema.

Zana haramu za uvuvi zilizoteketezwa ni pamoja na makokoro, vyavu zenye matundu madogo pamoja na nyavu zilizoshonwa kwa kutumia nyuzi aina ya timba (monofilament) ambazo haziozi kwa urahisi.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.