14 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ubalozi Cuba wamkatalia Emilian
 
2008-05-14 09:46:27
By Renatha Msungu

Ubalozi wa Cuba nchini umekataa maombi ya Shirikisho la ndondi za ridhaa (BFT) la kumpeleka bondia Emilian Patrick kufanya mazoezi nchini humo.

Balozi wa Cuba nchini, Dionisio Molina aliiambia Nipashe jana kuwa wamechukua hatua hiyo kutokana na muda kuwa mfupi.

Molina alieleza BFT hawakuwa makini katika maandalizi ya Emilian kutokana ukweli kuwa kujiandaa na michezo ya Olimpiki kwa mwezi mmoja ni kitu kisichowezekana.

Alisema kinachohofiwa ikiwa Emilian ataboronga kwenye Olimpiki basi watalaumu kambi ya kwao wakati ukweli ni kuwa muda ni mfupi.

Molina alieleza kuwa nchi yake hufanya vizuri katika michezo ya Olimpiki kutokana na kujiandaa kwa muda mrefu.

Alitoa mfano wa kuwa mabondia wa nchi yake watakaokwenda China, mwaka huu walianza kunolewa miaka miwili iliyopita.

Alishauri wanatakiwa wawe makini na michezo mikubwa, ambapo maandalizi ya muda mrefu huhitajika.

Cuba ni kati ya nchi zinazosifika katika ndondi za ridhaa duniani, ambapo hujizolea medali kibao za ndondi kwenye Olimpiki.

BFT walipanga bondia huyo aondoke nchini Juni 30, kuelekea nchini humo ili kujiandaa na michezo ya Olimpiki inayofanyika mwaka huu.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.