14 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Lweru Eagles yaitoa Ruvuma kwa matuta
 
2008-05-14 09:47:13
By Somoe Ng\'itu

Timu ya soka ya mkoa wa Kagera, Lweru Eagles jana ilifuzu kwa robo fainali baada ya kuilaza Ruvuma kwa penati 4-2 katika mechi ya Safari Lager Taifa Cup iliyochezwa Uwanja wa Taifa, jijini, Dar es Salaam.

Penati ndio zilitumika kuamua baada ya timu hizo mbili kuwa zimefungana 2-2 kwenye dakika 90 za kawaida.

Kipa wa akiba wa Lweru Eagles, Abdulrazak Jackson ndio aliweza kuibuka shujaa baada kufanikiwa kuokoa penati mbili wa Ruvuma.

Abdulrazak aliingia katika dakika za mwisho badala ya Kipa wa kwanza, Oddo Nombo ikiwa maalum kwa kasi hiyo.

Penati za Lweru Eagales zilizamishwa wavuni na David Charles, Martin Muganyizi, Juma Seif na Ladislaus Mbogo.

Zile za Ruvuma zilizamishwa wavuni na Ramadhan Kudundwa na Patson Chiwanga, ambaye ndio alikuwa mchezaji bora wa mechi.

Katika dakika za kawaida, ambapo Ruvuma ilionyesha soka safi na hasa kipindi cha pili mabao ya Kagera yalifungwa na Mussa Akunda na Paul Mgwai katika dakika za pili na 44.

Mabao ya Ruvuma yalizamishwa wavuni na Abdalla Ausi katika dakika ya 34 na lile la kusawazisha na Omar Kapilima katika dakika ya 90.

Kagera Sugar ilicheza dakika tatu za mwisho ikiwa na watu 10 baada ya Paul kutolewa kwa kuonyesha kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa mwenzake.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.